flash3

Friday 17 August 2012

Koffi Olomide ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.

Mwanamuzi mashuhuri nchini kongo(DRC) Anton Akgeba Makila Mabe maarufu pia kama Koffi Olomide aka Mopao Mokonzi, Aswekwa lupango na pia kafikishwa mbele ya mahakama.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kutumbukizwa rumande na kisha kufikishwa mahakamani mnamo hapo juzi.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Koffi alikamatwa kufuatia vurugu alilolizua katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi hapo jana asubuhi wakati aliposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.

No comments:

Post a Comment