flash3

Tuesday 21 August 2012

SAA YA NADAL YENYE THAMANI YA £241,000 ILIYOKUWA IMEIBIWA YAPATIKANA

Jumatatu ya wiki hii mcheza tennis Rafael Nadal alinyakua taji maarufu la French Open na sio tu kunyakua taji hilo kwa mara ya 7 bali pia kumaliza “uteja” uliokuwa umeanza kumnyemelea kutoka kwa Novak Djokovic hususani katika Grand Slam.
Lakini wakati Nadal akimenyeka uwanjani, katika hoteli aliyofikia kibaka mmoja alikuwa na kazi ya kufanya zaidi ya kuhudumia wateja. Jamaa akakwapua saa ya Nadal yenye thamani ya £241,000 (piga mwenyewe hesabu ujue hicho ni kiasi gani cha shilingi za kitanzania)-Pichani hapo juu ni mfano wa saa yenyewe.
Saa hiyo kutoka kwa watengeneza saa Richard Mille(saa ina jina hilo hilo). Wazazi wa mcheza tennis huyo ndio waliogundua kwamba saa ya mtoto wao imepotea. Na kwa sababu katika chumba cha hoteli hiyo alipokuwa amefikia Nadal na wazazi wake hakikuonekana kwamba kimevunjwa wala nini,mara moja wakajua kwamba huo utakuwa ni mchezo wa ndani kwa ndani. Walipofuatilia wakagundua kwamba jamaa mmoja anayesimamia baa hapo hotelini ndio aliingia kwani kadi yake ya kuingilia humo ndio ilitumika.
Jamaa akabanwa,akakubali kwamba ni kweli tamaa ilimzidi akakwapua saa hiyo.Akawaonyesha na alipoificha.Mchezo ukawa umekwisha,Nadal akaipata saa yake na jamaa ameshitakiwa kwa wizi

No comments:

Post a Comment