flash3

Tuesday 21 August 2012

NI KWELI KWAMBA KANYE WEST AME-TWEET PICHA YA UTUPU YA KIM KARDASHIAN?

 


Kila siku mtandaoni huwa kuna habari ambayo inakuwa kubwa kuliko zingine.Inakuwa gumzo. Leo Alhamisi neno lililozagaa ni kwamba Kanye West ame-tweet picha ya utupu(naked) na mpenzi wake wa sasa,Kim Kardashian.
Picha hiyo inamuonyesha msichana mwenye muonekano unaoshabihiana na Kim Kardashian kwa nyuma akiwa amekaa mahali kama hotelini hivi akionekana kula kitu kama tunda(kama unavyoiona hapo juu). Kwa mtazamo wa kawaida, ilionekana kabisa kwamba huyo ni Kim.Hata hivyo picha hiyo iliondolewa baadae ingawa tayari ilishaingia karibuni kila sehemu ya mtandao.
Swali likabakia ukweli uko wapi? Kwa mujibu wa TMZ, ingawa picha ilisemekana kutoka kwa Kanye West, ukweli ni kwamba ilikuwa ni prank tu ambayo ilianzishwa katika kitu kilichoitwa #WanksterWednesday. Na isitoshe kuna maneno kwamba hata huyo bibie anayeonekana katika picha hiyo sio Kim Kardashian.
ABC News baadae wakatanabaisha kwamba hiyo ni picha ya muigizaji wa filamu za X anayeitwa Amia Miley na yeye mwenyewe ndio aliwahi ku-tweet hiyo picha yake mwaka jana. Inasemekana Amia Miley anazo picha lukuki zinazomuonyesha akiwa namna hiyo na Kanye West aliwahi kui-tweet katika account yake.
Na mwenyewe Amia Miley amekubali kwamba hiyo picha ni ya kwake na hivyo ndivyo anavyopataga kifungua kinywa chake.
Of course Kanye amekanusha vikali kitu hiki na kukiita kichekesho tu! Kwa hiyo mchezo kwisha.Kanye hana hatia!Nguvu ya Twitter hiyo!

No comments:

Post a Comment