.Club ya Real Madrid imetangaza
kwamba Mchezaji Mkongwe wa soka wa Ufaransa Zinadine Zidane, atakuwa kocha
wa moja kati ya timu za vijana za Real Madrid huko nchini Uhispania.
Zidane mwenye umri wa miaka 40
ambaye alistaafu kucheza soka miaka sita iliyopita baada ya kumpiga
kichwa mchezaji Marco Materazzi kwenye fainali ya kombe la dunia ishu
ambayo ilimfanya aape kwamba hatorudi tena uwanjani, anataka kurudi
kwenye soka lakini akiwa kama kocha.Zidane ambaye amechapa soka ya kulipwa ndani ya Cannes, Bordeaux, Real Madrid na Juventus ambako kote huko alifanikiwa kuzigonga nyavu mara 95 toka ameanza kucheza soka mwaka 1988.
Zinedine Zidane atakuwa anaendelea na masomo yake ya ukocha wakati akiifundisha timu hiyo ya vijana na anatarajiwa kumaliza kozi hiyo mwaka huu.
Zidane anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Alberto Giraldez kama mkuu wa timu za vijana wa Real ingawa club hiyo haijathibitisha habari hizi mpaka sasa.
Mwiba huyu wa soka, amewahi kushinda taji la mchezaji bora ulimwenguni mara tatu.
Aidha Zidane ameshawahi kuapa kuwa mkufunzi wa soka siku moja na hata pia kuinoa timu ya taifa ya ufaransa.
No comments:
Post a Comment