flash3

Monday 11 March 2013

BAADHI YA MASTAR WA BONGO AMBAO NI SINGLE MOTHERS ..HAWA HAPA..!!

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’Alianzia kwenye filamu kisha akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu
wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa aliingia kwenye fani hizo kwa
ajili ya kujitafutia kipato ili kulea wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza
huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto mmoja kisha ndoa ikaota
 mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume mwingine
 ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema
kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo na sasa ameongezea muziki.
 Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday
Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa
kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi
 yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea
mwenyewe japo Mr Chuz huwa anampiga ‘tafu’.
SNURA MUSHI Alianzia kwenye uigizaji kabla ya hivi karibuni kujikita pia katika tasnia
 ya filamu. Ana mtoto mmoja wa kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito
 baba mtoto wake aliingia mitini. Mpaka sasa anamlea mwanaye
mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.
MAUNDA ZORROAlipata umaarufu kupitia muziki na baadaye akaongezea uigizaji.
Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika mwanaume
aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake,
mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.

No comments:

Post a Comment