flash3

Thursday 28 March 2013

HOUSEKEEPERS BRAZIL KULIPWA OVERTIME

house keepers
Baraza la Senate nchini Brazil, limepitisha bila pingamizi mswaada wa kihistoria unaowapa haki sawa wafanyakazi wa majumbani na wale na maofisini kote nchini.
Sheria hiyo mpya inafafanua idadi ya siku za kazi ambazo wafanyakazi hao pamoja na wapishi wanaweza kufanya kazi na hata kiwango cha ziada cha marupuupu watakachopata.

Mageuzi hayo ya kikatiba yataanza kutekelezwa wiki ijayo wakati ambapo rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff atatia saini mswaada huo.
Mabadiliko hayo huenda yakaongeza gharama ya kuwaajiri wafanyakazi wa majumbani kwa asilimia ishirini.
Kulingana na shirika la wafanyakazi duniani Brazil ndio nchi yenye idadi kubwa ya wafanyakazi wa majumbani duniani wakiwa milioni saba.

No comments:

Post a Comment