flash3

Friday 29 March 2013

LORD EYEZ KUHAIRISHA BABA LA BABA

baba
Kufuatia siku ya leo kwenye kalenda kuwa ijumaa kuu Rapper kutoka kampuni ya weusi Isac Maputo ‘Lord Eyez’ ametangaza kuhairisha mpango wake wa kudrop ngoma yake mpya inayoitwa ‘mapito’ feat Damian pamoja na video ya Baba la baba hadi siku ya jumatano.
Rapper huyo ambae hivi karibuni alikumbwa na misukosuko ya kesi za wizi wa vifaa vya gari la msanii mwenzake Ommy Dimpoz amesema kuwa mkakati wake ulikuwa ni kuachia kazi mbili kwa mpigo siku ya leo lakini kutokana na kwamba imeangukia siku ya sikukuu ameahairisha hadi siku ya jumatano.

Mkali huyo aliewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Ray C amesema kuwa kuhusu line za verse zinazo muombea Ray C na Mama yake kwenye wimbo wa mapito, fans wake watarajie kumuona mwanashost huyo akitokelezea kwenye kichupa cha wimbo huo kushow support na love ya kutosha.

No comments:

Post a Comment