flash3

Friday 29 March 2013

Jicho La Mfb Limekutana Na Luv Mumz Leo Hii........

Luv Muz Katika Poz....
Tumemuona  Luv Muz, Mwanzo Tukafahamu Kuwa Wazazi Wake Walifurahia Kumuita Mariam Farida Abdallah walipomzaa.
Mtoto Huyu Wa Kike Tumeongea Naye Mengi Hebu Fuatilia haya Mazungumzo Yetu Kupitia Sura Ya Kitabu.....
Yeye Alinikuta Na Ndipo Akanisabahi............... 
Na baada ya Salamu, Mumz Akaanza Kunishukuru Kwa Kupatia shavu Mziki Wake Kupitia kipindi Tafrija Select Cha Radio Pwani Ninachokiendesha...... Hapo Mimi Sikujibu.
Nikagundua Kuwa Ni Kizalia Cha Hapa Kisiwani Mombasa Pande Za King'orani Huyu Luv Mumz Alizaliwa 1989, Akalelewa Na taabu Kisha Baada Ya Kuvunja Ungo Mwanamuziki Skecher Wa Kikundi Cha Rude Boys Mjini Mombasa Akamposa Na Kisha Kumuoa Na Baada Ya Pandashuka Za Maisha Msanii Skecher Hakuliona Faida kuoa Msanii.........Hapa Mumz Hakutaka Kunielezea Sababu Nyingi Kwani Skecher Alimmwaga.
 Luv Mumz Akiwa Katika Poz...
Mumz Kwa Sasa Ana Watoto Wa Wili Wa Kike, Aisha Na  Rahima Wote Wako Chini Ya Ulezi Wa Mumz Kupitia Muziki, Du! Nikashangaa Kisha Nikameza Mate, Nikataka Kujua Kama Ana Kazi Nyingine Kando Na Muziki Mtoto Wa Kike Akanieelezea Kuwa Kwa Sasa Kila Kitu Ni Muziki.......Mumz Anapitia Mazito Ya Maisha Lakini Muziki Humfariji Na Pia Humlisha(Miss Indipendent huyu).
Kuhusu Muziki Wake Wa Hivi Karibuni 'Mapenzi Khalas' Aliutengeneza Kwa Producer Tee-T-Hits, Mumz Ananielezea Kwamba Hauzungumzii Mapenzi Yake Ya Zamani Lakini Hata Yeye Mwenyewe Anashangaa....mmmmm Mariam, Mariam Mariamu Nikamuita Mara Tatu Kwani Alikuwa Kimya, Nikagundua Kitu Lakini Nakibana......Mtoto Wa Kike Luv Mum Ana Mziki Wa Mashairi Mazito Na Sauti Yake Ya Mnato Aki Una Sababu Ya Kumsikiliza Na Kumpa Sapoti
Any Way Mengine Ni Kuwa Mumz Hupenda Kula Nini?......'Mimi Napenda Wali samaki fresh hivi mchuzi wachukuchuku na kama maini makavu yalokauka damu poa,juice ya ovacado hivi kishkishio' alinijibu hehehee Tukiyaacha Hayo Mumz Wapenda Mwanamume Wa Aina Gani? 'Du!' Kamaka.....'Hapo tutasameheana
Ni gumu hilo' akanijibu Sikutaka Kuendelea XANA
 MFB ENT YAMTAKIA KILALA HERI......

No comments:

Post a Comment