flash3

Tuesday 26 March 2013

OCTOPIZZO ASUKA NGOMA NYINGINE

OCTOPIZO
Mkareee wa michano Humu nchini Kenya rapa Octopizzo ambaye kila kukicha anajichimbia studio akipika vibao vipya hivi sasa amejipanga zaidi kufanya Kolabo na wanamuziki wa kimataifa baada ya hivi karibuni kuanika wazi projekti zake mpya kwa mashabiki wake.
Rapa huyo ametoa kibao kipya alichokibatiza jina ‘We are One’ akishirikiana na bendi moja maarufu kutoka nchini Sweden inayofanya miondoko ya rock inayoitwa ‘Chef’s Special’ akisema kuwa muda wowote kuanzia sasa anatarajia kukiachia hewani.

Octopizzo ambaye hivi karibuni alitumbuiza katika onyesho moja la Dj Final Cut’s and Frankie’s Hip-Hop Culture show imeelezwa kuwa kuna kazi mpya ambayo pia amefanya na wasanii wanoliunda kundi la ‘Just A Band’ hivyo mkae mkao wa kula kwa kazi hizo mpya.

No comments:

Post a Comment