flash3

Thursday 21 March 2013

LULU AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA TANGU ATOKE GEREZANI

KWA mara ya kwanza tangu atoke mahabusu ya Gereza la
Segerea, Dar kwa dhamana, staa wa filamu na video za
 wasanii wa Bongo Fleva, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au Lizy
 amefunguka juu ya uhusiano wake na aliyekuwa mwandani
wake, marehemu Steven Kanumba na kusababisha
 gumzo kubwa mitandaoni.
Huku akipiga picha za pozi kwa mara ya kwanza tangu
 atoke selo, Lulu alifunguka wikiendi iliyopita kupitia
 ukurasa wake katika mitandao ya Instagram na Twitter kuwa
 Kanumba alikuwa zaidi ya baba, kaka, mpenzi, mume, ndugu
 na rafiki hivyo hataacha kumlilia maisha yake yote.

Huku akitanguliza picha ya marehemu Kanumba enzi za uhai
 wake akipokea moja ya tuzo zake, Lulu aliandika:

“Ulikuwa zaidi ya baba, kaka, mpenzi, mume, ndugu na rafiki…
sitaacha kukulilia katika maisha yangu yote!! R.I.P
daddy yangu Steven Kanumba.”
Ndani ya muda mfupi, kauli hiyo ya Lulu ilipata maoni mengi
 huku baadhi ya watu wakimpa pole kumtia moyo na wengine
wakijibizana kwa hasira juu ya ishu hiyo.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia marehemu
Kanumba ambayo inatarajiwa kuanza
kuunguruma muda wowote.

No comments:

Post a Comment