flash3

Friday 29 March 2013

LOVE N’ POWER KUTOKA APRIL 7/2013

Love-Power
Baada Ya Mtandao Huu Kuangazia Kuwa Sanamu Ya Kanumba Kutarajiwa kutundikwa Huko Bagamoyo Nchini Humo Sasa Kingine Kumuhusu Marehe Kanumba Ni Kuwa Filamu ya mwisho ya marehemu inayoitwa “Love and Power” inatarajiwa kuingia sokoni mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Taarifa hizo zimetolewa hivi karibuni na Seth ambae ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba wakati alipokuwa akihojiwa Na chumba kimoja cha Habari Nchini Tanzania.
Seth ambae kwa sasa ameanza kuendeleza kampuni ya The Great Steven K’ ameeleza kuwa filamu hiyo imechukua muda mrefu kumalizika kutokana na wahusika wakuu Kanumba na Sharomilionea kufariki dunia.
Aidha ameongeza kuwa kulikuwa na changamoto nyingi hasa katika ku edit filamu hiyo kutokana na kwamba baadhi ya scene zinazo muonyesha marehemu Steven Kanumba zimekua zikishabihiana na uhalisia wa jinsi kifo chake kilivyotokea.
Filamu hiyo ambayo ilianza kutengezwa tangu mwezi march mwaka jana ndio movie ya mwisho ya muigizaji Steven kanumba kabla ya kifo chake.

No comments:

Post a Comment