flash3

Thursday 28 March 2013

Susu Aangazia Mataifa Ya Ughaibuni.

Susumila Ni Jina Ambalao Hapa Pwani Na Kenya Nzima Kwa Ujumla, Hakuna Isiye Lijuwa Ikizingatiwa kuwa ni jina tajwa na limekuwa vinywani mwa wengi.
Hata hivyo ni jina linalomilikiwa na msanii wa kizazi kipya Yusuf Kombo kizalia cha pwani kaskazini.
Mfb ilipokuwa ikimfuatilia leo hii imegundua kuwa mwezi huu wa tatu tarehe 13 aliajaliwa kupata mtoto wa kiume wa pili na kwa hilo roho yake imefurahi.
Akizungumza na sisi kupitia njia ya simu susu alikuwa pande za Chumani ambako anamiliki nyumba pamoja na biashara zingine zake.
Baada Ya kuingia ndani sana katika gumzo letu, kuhusu familia yake, machache tuliyoyapata nikuwa mkewe pia nishabiki wake sugu na hasa yeye hupenda traki "Nikupe Nini".
Susu alituelezea zaidi kuhusu muziki wake na akasema hivi karibuni anatarajia kuachilia traki mpya kazi ikisalia ya producer J Krak Ndani Ya Studio Za Krak Sounds.
Akigusia Swala la mauzo ya muziki wake, susu asema kuwa yuko mbioni kuuza muziki wake katika mataifa ya kughaibuni ikizingatiwa kuwa tayari ashachukuwa kandarasi na kampuni moja ya mauzo Ya muziki kimataifa, kampuni ambayo huuza miziki kupitia mitandao.
Kando na Hayo, Susu Hujihusisha na maswala ya kijamii hasa yeye hupendelea kuwatembelea Watoto ambao Hawajabahatika(opharnage Homes) Pamoja na Wagonjwa huku akisema kuwa lazima jamiiifaidike na mfuko wako.
Susumila atasalia kuwa msanii mkongwe hapa pwani amabaye jina lake bado nitamu ndani ya vinywa vya wengi...kilala heri kwa kazi zake.........

No comments:

Post a Comment