flash3

Friday 29 March 2013

PREZZO KUMUENZI GOLDIE KWA KUMUIMBIA

prezzo
Zikiwa zimepita siku nyingi za ukimya kwa takriban mwezi mmoja tangu kufariki kwa msanii maarufu wa kibao cha ‘Skibobo’ Goldie Harvey wa nchini Nigeria, msanii Prezzo anatarajia kufanya ngoma mpya itakayokuwa maalum kwa ajili ya kumuenzi mpenzi wake.
Prezzo alikumbwa na fedheha baada ya kukataliwa na familia ya marehemu Goldie kuhudhuria maziko ya mpenzi wake huyo Jijini Lagos nchini Nigeria baada ya kugundulika kuwa Goldie alikuwa ni mke wa mtu na familia haikutaka kuibuka kwa mvutano wakati wa kumzika mpendwa wao.
Rapa huyo amesema kuwa ngoma hiyo mpya inayotarajiwa kutoka muda si mrefu ya kumuenzi mpenzi wake ameibatiza jina “MY NAIJA GIRL”.

No comments:

Post a Comment