flash3

Tuesday 26 March 2013

LUPE FIASCO:MUZIKI WA VURUGU HUPELEKEA VITENDO VIOVU

MC Lupe Fiasco ametumia akaunti yake ya twitter, siku ya jumapili kuongea dhidi ya maudhui yanayochochea vurugu katika vyombo vya habari na katika muziki wa rap kwa ujumla
katika tweets zilizofatana ndani ya muda wa dakika 20, Lupe anadai kuwa uhusiano wa dhahiri kati ya vurugu katika muziki na ulimwengu wa kweli.
aliendelea kuwaambia rapppers ambao anahisi wanatumia  picha za vurugu katika mziki wao  na kusema wanahitaji kuchukua jukumu kwa maudhui wanayozalisha na madhara yake katika jamii



kuomboleza kwa mwenyeji huyo wa  Chicago kupitia mitandao ya kijamii, inaonekana kusababishwa na vurugu zinazoendelea katika mji wake pamoja na habari iliyoripotiwa kuhusu mauaji ya mtoto mdogo, Georgia.
Hii sio mara ya kwanza kwa Lupe kutoa maoni yake juu ya kuamini kuwepo na uhusiano kati ya vurugu zilizoko katika muziki na vurugu za mtaani, mwaka jana alimchana rappar Chief Keef na kusema utamaduni anaouwakilisha ni wa vurugu na kuwa anamtisha kwa utamaduni huo.

No comments:

Post a Comment