flash3

Monday 11 March 2013

Producer Mdogo Zaidi Mombasa.........

 (Producer Collinsaca Akiwa katika Kazi Nzito)
Collins Mwaisaka Maarufu Kama Consaka Ni Kijana Mzaliwa wa ardhi ya pwani kaskazini, asiyekuwa na zaidi ya miaka 25 na ambaye ameingilia kazi hii ya kutengeneza muziki maarufu kama Production kwa kasi ya ajabu sana.
Colinsaka Amefanyia kazi studio nyingi Pwani Hii Ikiwemo E-30 Recs Iliyoko Mtwapa, na Kwa sasa Yupo chini Ya studio Za Houz Of Grace Zilizoko Mtopanga.
Colinsaca Amefanyia kazi Wasanii Wakubwa Pwani Akiwemo Nyota Ndogo, Alkenia Luv, Jay Star Na wengineo ambao ndani ya 254 hii ya pwani Wanasikika na Kushika Hewa Nzima ya Afrika Mashariki.
 Akizungumza na mtandao huu, Colinsaca asema kuwa fani ya muziki pwani yastahili malezi na hii ina maana kuwa ushurikiano baina ya msanii, producer, presenter pamoja na promoter ni muhimu sana.
Aidha amesisitiza kuwa wanamuziki wanafaa, kuwa na ubunifu zaidi ili kushindana production za kimataifa.
Wakati uo huo aliwaomba maproducer wenzake kujifunza muziki kiteknolojia, hii nikumaanisha kuwa lazima wajue ala zote za muziki na na kupambana na teknolojia ya production pale imefika.

No comments:

Post a Comment