flash3

Tuesday 26 March 2013

DR. JOSE UTAJIRI SI KITU

jose chamilion
Nyota wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone ameamua kuweka wazi suala la yeye kukubaliana au kutokubaliana na kuwekwa kwenye orodha ya wasanii nyota matajiri barani Afrika kutokana na utajiri wake alioupata kupitia muziki wake.
Jarida moja la burudani nchini Uganda limeandika habari za Chameleone akisema kuwa hayupo tayari kunyanyaswa na mtu yeyote kutokana na kumiliki utajiri wake alionao kwani yeye kazi yake kubwa ni kuwapa watoto elimu yenye ubora kupitia muziki wake na sio kujigamba kuwa ni tajiri.

Chameleone ambaye pia anatarajia kuzindua albamu yake ya nne aliyoibatiza jina Badilisha mwezi ujao jijini Kampala amemalizia kwa kusema kuwa yeye si kitu si chochote linapokuja swala la utajiri kwani utajiri alionao upo kwa mashabiki wake tu.

No comments:

Post a Comment