flash3

Friday 22 March 2013

MSANII HUYU MATATANI KWA UJAMBAZI...

 STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni
aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar
 baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake
 (jina tunalo).

Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa
 siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango
 nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na
askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa
 kwa ujambazi.

Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni
wapi dada huyo amevunjiwa  au kitu gani alichoibiwa, askari
walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana

No comments:

Post a Comment