flash3

Monday 22 October 2012

ANT EZEKIEL AFUNGUKA NA KUWEKA WAZI JUU YA KITCHEN PARTY NA SEND OFF

Zimepita siku kadhaa toka msanii wa Bongo movie afunge ndoa yake sasa bhana dzain tukaamua kumtafuta na afunguke je ni kwanini aliamua kufanya ndoa wakati siku zote tamaduni au mila za kwatu hapa Bongo kama tunavyofahamu mtu siku zote mtu anapotaka labda kuolewa  basi ni lazima apitie labda Kitchen party akitoka hapo Send off baada ya hapo ndipo mwisho wa siku tunakuja kwenye upande wa ndoa.Sasa chakushangaza msanii huyu wa Bongo movie yeye amefanya ndoa tu.Sisi kama watu wa media baada ya kuona kitu kama hiki
tuliamua kumuita na atuambie kuhusiana na kitu kama hiki huyu hapa anafunguka kama ifuatavyo"“Ni mchumba wangu na ndiye mwenye maamuzi nikaamua nifanye hivyo,” ameiambia ‘Movie Leo’ ya Clouds FM. “Naweza kusema bado yaani siko sawa mpaka nihakikishe hivyo vitu vyote vimeenda vimepita salama maana unajua shughuli yoyote hata kama ndogo lakini lazima unajua yaani unakaa ni pressure yaani sijui itakuaje sijui itakuwa vipi? Kwahiyo naweza kusema kwasababu ni mwanzo kwahiyo bado kiukweli naona yaani huko mbele kutakuaje.”
Baada ya hapo msanii huyu pia aliimbia Movie leo ya clouds fm kwamba kwasasa ana michakato ya kuanza na hatua ya mwisho ya harusi na kurudi nyuma yaani kuiflashback, muigizaji huyu pia alifunguka na kueleza  jinsi Kitchen Party za Send-off zitakavyokuwa,nataka nifanye vitu vya tofauti na kila kitu nataka kiwe tofauti sana na vile watu ambavyo wameshazoea kuviona au wamewahi kwenda katika masherehe mbalimbali ya maharusi.Hayo ndiyo maneno ya msanii wa bongo movie baada ya kumuuliza maswali kwamba ni kwanini amechukua uamuzi wa kufanya ndoa kabla ya Send off pamoja na kitchen party.

No comments:

Post a Comment