flash3

Tuesday 23 October 2012

KESI YA LULU MPAKA TAREHE 5 NOVEMBA

MSANII  wa filamu nchini Tzee, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu lilikofikia jalada la kesi.
Lulu aliuliza swali hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stuarti Sanga baada ya Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi wake haujakamilika duuuhhh!!!!!


Baada ya Sekwao kueleza hiyo, Lulu alinyoosha mkono na kuweza kuhoji kwamba jalada la kesi inayomkabili lilikofikiani wapi??
 Baada ya hapo Hakimu Sanga alimuuliza Wakili Sekwao iwapo anauliza jalada halisi au la kudurufu. 


Wakili Sekwao alimwambia Hakimu Sanga kuwa, anaulizia jalada halisi.Hakimu Sanga alimwambia Lulu kuwa jalada halisi limekwisharudi  na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena.
 Msanii huyu wa bongo movie anatuhumiwa kwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kwa kutenda kosa hilo tarehe 7 mwezi wa April , mwaka huu nyumbani kwa Late Kanumba, Sinza, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment