flash3

Monday 22 October 2012

DOGO JANJA SOON KUFANYA COLLABO NA PREZZO

Msanii kutoka Mtanashati Entertainment,Dogo Janja sasa hivi yuko mbio kwa kufanya kazi na wasanii wakali wa hapa African.Japokuwa ni msanii mdogo sana lakini anachotaka ni mabadiliko katika mziki wake wa hapa Bongo Land.Kama unakumbuka kipindi cha nyuma alishawahi kufunguka na kusema kwamba ndoto zake siku anatamani zile kama level za mtu mzima A.Y ambaye hivi sasa msanii huyu anajulikana mataifa mbalimbali kwa kupitia mziki wake.Sasa ile ndoto ya Dogo janja bhana ya kutaka kuwa kama A.Y dzain kama ndiyo hii baada ya kufunguka na kusema kwamba kwasasa amefanya mazungumzo na Prezzo kwa hiyo soon wanatarajia kuingia studio na kufanya kazi kwa pamoja lakini sasa Dogo janja akuamua kuweka wazi jina la ngoma hiyo kwani alisema mpaka itakapofahamika kwamba wanafanya ngoma gani ndipo ataweza kutaja jina la ngoma pamoja na jina la studio ambayo watafanyia mpango mzima wa vocal na mixing.Hivyo ndivyo Dogo janja aliamua kufunguka kuhusiana na collabo ambayo atamuhusisha mtu mzima Prezzo kati ya mwezi wa 11 au 12.

No comments:

Post a Comment