flash3

Thursday 25 October 2012

DIAMOND ADAI KUOA NI BAADAYE SANA

Msanii wa Bongo fleva, Naseeb Abdul,  a.k.a Diamond wa wasafi  siku za hivi karibuni alifunguka na kusema kwamba hana mpango wa kuoa siku za karibuni kwa kuwa bado anahitaji sana mapenzi ya karibu na mama yake.
Akihojiwa na vyombo vya habari hapa Tzee, Diamond alisema kumekuwa na maneno mengi sana yanayozagaa kuwa hivi karibuni atamuanika mchumba wake anayetaka kufunga naye ndoa, jambo ambalo si la kweli.
Diamond, ambaye unaweza kusema ndiye mwanamuziki anayefunika kwa sasa katika miondoko ya Bongo fleva, kutokana na ngoma zake kupendwa na mashabiki wengi hapa Tzee hata nje ya Tzee, alisema kwamba mbali na kuhitaji mapenzi kwa mama yake, pia ushauri wake ni jambo la muhimu katika kila jambo analotaka kulifanya.
“Unajua mimi ninampenda sana mama yangu na ndiye kila kitu kwangu, hivyo najikuta hakuna kitu ninachoweza kufanya bila kumjulisha, hivyo kuwa naye mbali kwa sasa itakuwa ngumu,” alisema.
Akizungumzia kuhusu uhusiano wake na aliyewahi kuwa na mahusiano na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, alisema kwa sasa ni rafiki yake wa kawaida tu, si mpenzi na wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali.
Kwa mujibu wa Diamond, matatizo yote yaliyotokea huko nyuma, wameshasameheana na sasa hivi wanaiva vilivyo.
Diamond na Wema walishawahi kuwa wapenzi na kujikuta wakimwagana mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo habari zao ziliteka vyombo mbalimbali vya habari, hasa pale mwanamuziki huyo alipofanya onesho lake Mlimani City na kuzikataa fedha alizokuwa akipewa  na mwanadada huyo.Lakini kwasasa Diamond anatuhumiwa kwamba anamahusiano na mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Najma sema msanii aliendelea tu kusema kwamba Najma si mpenzi wake ila ni rafiki tu Duuuuhh!!!!! baada ya hayo ndipo akaamua kusma kwamba suala la kuoa sio wakati huu ni baadaye sanaa .

No comments:

Post a Comment