flash3

Wednesday 24 October 2012

‘MFU’ AREJEA SIKU YA MAZISHI YAKE WAKATI ‘PACHA’ WAKE AKIWA KWENYE JENEZA

Gilberto aliporejea siku ya ‘mazishi’ yake.
FAMILIA ya Gilberto Araujo, mkazi wa jiji la Sao Paulo, Brazil, ilikuwa haijamwona kwa muda wa miezi minne baada ya polisi kutangaza Jumapili iliyopita kwamba tayari alikuwa ameuawa.
Familia ilipokuwa imejitayarisha kwa 'mazishi' yake.
Hali hiyo ilimfanya kaka yake, Jose Marcos Araujo, siku ya Jumanne kwenda mochwari na kuchukua mwili wa Genivaldo Santos Gama, mtu…
Gilberto aliporejea siku ya ‘mazishi’ yake.
 Hata hivyo, ‘marehemu’ Gilberto Araujo  (41) alipata habari kutoka kwa rafiki yake wakiwa mitaani ambapo alimwambia kwamba familia yake ilikuwa inatambua kwamba alikuwa amekufa.
Kilichofuatia ni kwamba Gilberto alikwenda nyumbani kwao na kukuta watu wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya mazishi yake na kuna jeneza lenye mtu ndani ambaye waliamini alikuwa ni yeye.
Gilberto akiwa na mama yake, Marina Santana, baada ya kusemekana alikuwa amekufa.
Mkanganyiko huo ulitokana na kwamba Gilberto na Gama wote walikuwa ni waosha magari, hivyo polisi waliipotosha familia ya Gilberto kwa kuwaambia ndugu yao ameuawa, badala ya kuiambia familia ya Gama.
Hata hivyo, watu hao wawili pia wanasemekana wanafanana, na ndiyo maana kaka mtu akakosea na kuchukua maiti ya Gama.
Pia tatizo jingine ni lile la kutoonekana kwa Gilberto kwa muda wa miezi minne.

Familia ilipokuwa imejitayarisha kwa 'mazishi' yake.
Hali hiyo ilimfanya kaka yake, Jose Marcos Araujo, siku ya Jumanne kwenda mochwari na kuchukua mwili wa Genivaldo Santos Gama, mtu ambaye anafanana sana na ndugu yake mwosha magari aliyesemekana kuuawa.
Hata hivyo, ‘marehemu’ Gilberto Araujo  (41) alipata habari kutoka kwa rafiki yake wakiwa mitaani ambapo alimwambia kwamba familia yake ilikuwa inatambua kwamba alikuwa amekufa.
Kilichofuatia ni kwamba Gilberto alikwenda nyumbani kwao na kukuta watu wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya mazishi yake na kuna jeneza lenye mtu ndani ambaye waliamini alikuwa ni yeye.

No comments:

Post a Comment