flash3

Thursday 4 April 2013

BEBE COOL MAMBO MAGUMU

bcool2
Mambo yameonekana kumuendea kombo msanii Bebe Cool wa nchini Uganda hasa baada ya mvua kali kumharibia onyesho lake la hivi juzi huko Kiwatule, na kabla machungu hayajamuisha, mapaparazi wamenasa tukio lingine ambapo wamekuta Hummer ya msanii huyu ikiwa imefungwa mnyororo.
hurmer
Bado sababu ya kufungwa kwa gari hili inafuatiliwa hasa kutokana na eneo lenyewe la tukio kutokuonyesha dalili yoyote kwamba huenda msanii huyu alilipaki sehemu isiyotakiwa, kitu ambacho kinasababisha wengi kuamini kuwa labda ni mtu anayemdai ameamua kufanya hivyo.
Gonga continue reading kuendelea..

Msanii huyu pia kupitia mtandao amekiri kupata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 80 za Uganda hasa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha kupata idadi ndogo ya watu katika shoo, ila bado hajasema chochote kuhusiana na gari kupigwa mnyororo.

No comments:

Post a Comment