flash3

Friday 26 April 2013

CAMPMULLA: KUNDI HALIJAVUNJIKA

Camp Mulla
Baada ya rumors kutembea all over the way kuwa kundi la camp mulla nchini Kenya huenda likavunjika, wakali hao wametoa ufafanuzi kuwa lengo si kutengana isipokuwa kujipa nafasi kufanya solo project.
Mmoja wa memba wa kundi hilo, Shappa Man, ameweka wazi kuwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo wasanii wa kundi hilo watakuwa wakiachia tu solo singles ambazo nia na madhumuni ni kutoa ile fikra ya kwamba kundi hilo linavunjika bali wanaendeleza fani zao nje ya kundi.
Shappa man amemalizia kwa kuelezea kuwa hii itakuwa ndio safari nzima ya kuweza kuelekea katika kazi za nje ya kundi na itasaidia pia kulipa sifa kundi hilo kutokana na watu wengi kulikubali kuanzia ndani na nje ya nchi kwani tayari wamejijenga kimataifa zaidi.

No comments:

Post a Comment