flash3

Friday 12 April 2013

BOBI WINE AWAKUBALI GOODLYFE

radio & wisle
Msanii Bobi Wine ametokea kuwamwagia sifa kem kem wasanii wakali kutoka Goodlyfe Moze Radio na Weasel ambao hivi sasa wamemaliza ziara yao ndefu ya muziki iliyobatizwa jina Europe Easter tour ambako waliwapagawisha mashabiki kibao nchini Denmark.
BOBI
Bobi Wine (Pichani)
Bobi Wine amesema kuwa pamoja na kwamba kuna baadhi ya watu wana utofauti na wasanii hawa amediriki kuwakubali kwa vipaji na uzoefu wao katika kutumbuiza na kuutangaza muziki wao kimataifa zaidi.
Gonga continue reading kuendelea..

Aidha, Bobi Wine anatarajia kuwasindikiza wasanii hao katika tamasha la uzinduzi wa albamu yao ‘OBUDDE’ linayotarajia kufanyika tarehe 10 mwezi ujao ambapo baadhi ya wasanii wakiwemo Juliana Kanyomozi, Iryn Namubiru na wengineo wanatarajia kuwapa sapoti washkaji hao ambao pia wapo mbioni kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya onyesho la muziki.

No comments:

Post a Comment