flash3

Friday 12 April 2013

NONINI ASIKILIZIA AHADI ZA KENYATTA

Nonini
Nyota wa muziki wa Genge nchini Humu Nchini Nonini amesema vijana wa Kenya wanakila sababu ya kuwa na matumaini na serikali mpya ya awamu ya nne iliyoingia madarakani rasmi juzi.
Katika ukurasa wake wa facebook Nonini amesema fungu la shilingi bilioni 6 lililoahidiwa kutengwa kwa ajili ya Mfuko wa Vijana na Wanawake ni ishara njema.
Pia Nonini amesema anaanza kuhesabu muda wa ahadi zilizotolewa kutekelezwa ndani ya siku 100 za kwanza za serikali ya rais Uhuru Kenyatta ikiwemo kutoa laptop kwa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule za msingi za umma.
Katika posti yake hiyo amesema leo ni siku ya kwanza bado siku 99, 'Daah Nonini upo makini katika kufuatilia ahadi! kazi kwako Rais Kenyatta kutimiza ahadi maana ahadi ni deni.

No comments:

Post a Comment