flash3

Friday 26 April 2013

URBUN BOYS: KUNDI LA MZIKI LINALOFANYA POA ZAIDI RWANDA

Urban-Boys
Kundi la muziki la Urban Boys la mjini Kigali nchini Rwanda limefyatua kibao chao kipya walichokibatiza jina Kelele ambapo kiongozi wa kundi hilo Humble Jizzo ameweka wazi kuwa tayari kichupa hicho ambacho kinafanyiwa utayarishaji na prodyuza Ark Menz ,kinatarajia kuwa hewani muda wowote kuanzia sasa.
Kundi hilo lenye wasanii watatu wa kiume wakiwemo James Manzi, aka Humble Jizzo, Safi Niyibikora, aka Safi Lee na Muhammed Nshimi-yimana, anayejulikana kama Nizzo wamesema kuwa wana imani na prodyuza huyo kwani aliwahi kuwatayarishia wimbo wao unaoitwa ‘Bibaye’, uliowahi kushinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka huu wa 2013.
Urban-Boys
Aidha prodyuza huyo aliwahi pia kufanya kazi na nyota wengine wa Uganda wakiwemo Grace Nakimera, Iryn Namubiru, Weasel & Radio na msanii wa kike wa Uganda mwenye makazi yake nchini Uingereza Fyonna Nsubuga, na wengineo.

No comments:

Post a Comment