flash3

Thursday 4 April 2013

CHEGE AKUTWA NA BALAA LINGINE

chege
Star wa single mpya ya ‘uswazi Take away’ Chege Chigunda amefunguka kuhusu tukio la majambazi ambao wamevamia nyumbani kwake wakiwa na silaha za moto na kuiba vifaa vya gari lake ambavyo vina thamani ya takribani shilingi milioni mbili.
Chege amesema hawezi kumtuhumu mlinzi wake kwasababu anamwamini hawezi kumwibia na licha ya hayo star huyo aliongeza kuwa waliofanya tukio hilo walidhamiria kurudisha harakati zake nyuma na ndio sababu walimtishia hata mlinzi wake kwa bastola.
Gonga continue reading kuendelea..

Mambo magumu yamekua yakimkumba msanii huyo katika kipindi cha muda mfupi licha ya ajali iliyo haribu gari lake vibaya mwaka jana (2012) maeneo ya Temeke Dar es salaam wakati alipojaribu kumkwepa muendesha pikipiki.
Gari-la-Chege-baada-ya-ajali
Hivi karibuni Chege Chigunda alitambulisha video ya wimbo wake mpya unaojulikana kama Uswazi ‘Take away’ na kama ilivyo kawaida ya msanii huyo kufanya vizuri track hiyo imeanza kutamba kwenye vituo mbalimbali vya televisheni hapa nchini.

No comments:

Post a Comment