flash3

Tuesday 23 April 2013

BEN POL: SIWEZI KUSHINDANA NA LADY JAYDEE

ben_pol
Baada ya kuwepo tofauti kati ya komando lady Jaydee na Benard Paul aka Ben pol kitaa Ben Pizee, limeibuka jipya baada ya teaser ya wimbo mpya wa Ben Pol uitwao ‘Jikubali’ kutoka na star huyo kuskika akiimba kuwa anampenda lady Jaydee.
Mkali huyo aliamua kutoa ufafanuzi kupitia mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu kupitia kituo kimoja cha radio hapa nchini akidai kuwa licha ya tofauti iliyojitokeza hivi karibuni hana tatizo sana na Komando.
“Sina tatizo na line niliyoimba kuwa nampenda Jide by the way wimbo wenyewe niliurekodi tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2013 kabla hata ya kutokea hizo tofauti”. Said Ben Pol

No comments:

Post a Comment