flash3

Wednesday 10 April 2013

RIRI & BROWN MAPENZI YA KIHINDI

Riri-Chris-Brown
Hadi sasa bado ni kitendawili ambacho kinasubiriwa kuteguliwa kutokana na uhusiano wa Chris Brown na Riri ambao hivi majuzi imeonekana Chris ameanza wivu wa kupindukia baada ya kuanza kumsakama Rihanna juu ya kuachana kabisa kuwasiliana na vidume vyake vya awali.
Habari zilizopo hivi sasa ni kwamba mwanashosti Rihanna baada ya kuona dalili hizo za laazizi wake Chris ameamua kuachana kabisa na maswala ya kimapenzi na kuamua kuwa kivyake zaidi ambapo hivi sasa amefocus zaidi na ziara yake kubwa ya muziki ya ‘Diamonds Tour’.
Gonga continue reading kuendelea..

Aidha mwanashosti huyo yupo pia mbioni kuzindua kampuni ya manukato pamoja na kutangaza nembo yake ya maswala ya mavazi na urembo wakati huo inasemekana kuwa Rihanna hajaweka wazi kuhusu kuanza maisha ya kuwa singo ila dalili za mvua ni mawingu baada ya shosti huyo kuanza kuwa kivyake.

No comments:

Post a Comment