flash3

Thursday 25 April 2013

JACKIE APPIAH KAOLEWA TENA

appiah
Mwigizaji mkali wa Ghana, Jackie Apiah ambaye miezi michache iliyopita alipewa talaka kwenye ndoa yake iliyojaa migogoro, kwa sasa imefahamika kuwa anajipanga kwa ajili ya kufunga ndoa tena.
Jackie ambaye ni mama wa mtoto mmoja, safari hii anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake kutoka nchini Naijeria, Bobby Obodo ambaye naye pia ni mwigizaji, na hii ni baada ya ndoa yake iliyodumu kwa miaka 5 na baba mtoto wake, Peter Agyemah kuvunjika.
Jackie pamoja na Bobby kwa sasa wamezidisha ukaribu wao kwa kiasi kikubwa na tayari taarifa zinaweka wazi kuwa Bobby amekwishaji tambulisha kwa familia ya Jackie na kupokelewa vizuri.

No comments:

Post a Comment