flash3

Wednesday 24 April 2013

UFARANSA YAHALALISHA NDOA ZA MASHOGA BAADA YA MJADALA MKALI

Christiane Taubira, Waziri wa sheria wa Ufaransa 
Watunga sheria wa Ufaransa wamehalalisha ndoa za jinsia moja baada ya miezi ya mjadala mkali  na maandamano ya mitaani yaliyopelekea mamia kwa maelfu  kuja Paris.
kura 331 - 225 za siku ya juma nne zimeangukia kwa walio wengi ndani ya bunge ambao ni Socialist. waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira,amesema ndoa ya kwanza kufungwa itaweza kuwa mapema mwezi june.
wanaopinga sheria hiyo wanasema, Ufaransa haiko tayari kuhalalisha ndoa za jinsia moja, na kura zinaonyesha kuwa wafaransa wamejitenga juuu ya swala hilo.
mamia ya askari walimwagwa nje ya viwanja vya bunge kabla ya kura hizo kupigwa, kwa maandalizi ya kama kungekuwa na maandamano kuzunguka jengo la bunge na kando kando ya mto Seine.
Ufaransa ni nchi ya 14 ya kuhalalisha ndoa za mashoga, na kura ya Jumanne imekuja wiki moja baada ya New Zealand - kwa utata kidogo sana - kuruhusiwa wanandoa wa jinsi moja kuoana.

No comments:

Post a Comment